Kampeni/Timu ya Bidhaa ya WMF

This page is a translated version of the page Campaigns/Foundation Product Team and the translation is 60% complete.
Outdated translations are marked like this.
Community Content Campaigns

Timu ya bidhaa ya Kampeni ya Wakfu wa Wikimedia inalenga kuboresha uzoefu wa Wikimedia campaigns. Timu iliundwa mnamo 2021, na inaangazia mahitaji ya waandaaji wa kampeni na washiriki. Tunapanga kuongeza na kuboresha vipengele katika mfumo ikolojia wa kampeni kadri muda unavyoenda.

Miradi

The team has built various features for the CampaignEvents extension, includingː

  • Event registration: We have created an on-wiki tool that lets organizers add a 'Register' button their event page. The event registration solution also includes many other features, such as: the option for participants to register privately, automatic confirmation emails after registration, integration with the Programs & Events Dashboard, and more.
    • Status: Available on all wikis that have the CampaignEvents extension enabled.
  • Collaboration List: The Collaboration List is a global, automated list of events on events on the wikis, and it is also a list of WikiProjects on a given local wiki. Organizers don’t need to do any extra work for their event or WikiProject to appear on the Collaboration List. As long as they use Event Registration for their event, their event will appear in the Collaboration List. Meanwhile, as long as their WikiProject has a Wikidata item, the WikiProject will be included in the Collaboration List. The Collaboration List also includes filters, so users can easily search for specific types of events.
    • Statusː Available on all wikis that have the CampaignEvents extension enabled.
  • Event discovery (invitation lists): The event discovery project aims to create or improve tool(s) that make it easier for editors to learn about campaign events on the wikis. For this project, we are developing an Invitation List tool, which allows organizers to generate a list of contributors who they may want to invite to their events.
    • Status: Available on all wikis that have the CampaignEvents extension enabled.

Tunapanga kuanza na miradi hii, na kuona kile tunachojifunza kutokana na kufanya kazi na Waandaaji wa Matukio.

Iwapo ungependa kupata taarifa zetu motomoto kuhusu kule tunakotaka kufika na maendeleo ya kiufundi tafadhali jiunge na jiandikishe ili kupata taarifa zetu hapa chini.

Fuatilia kazi yetu

Telegram group

You can join the Event Organizer group on Telegram, which is a multilingual chat group for organizers of events in the Wikimedia movement. We post announcements and updates about our team's work in the Telegram group, and we also take in feedback, such as feature requests and bug reports. Organizers are encouraged to share their updates, tools, and ideas in the group too.

Newsletter

Tutakuwa tukituma majarida ya taarifa kuhusu kinachoendelea ya mara kwa mara (sanasana kila mwezi) kupitia Ujumbe kwa wengi.

Taarifa zilizopita

Ikiwa ungependa kujiandikisha ili dondoo hizi zitumwe kwenye ukurasa wako wa mtumiaji, tafadhali jiandikishe hapa!

Office Hours


Timu ya bidhaa: Utangulizi

Kuanzia Julai 2021, Wikimedia Foundation ina timu ya bidhaa ya Kampeni itakuwa ikitatua mahitaji ya waandaaji na washiriki wa kampeni. Timu ya bidhaa ya Kampeni itakuwa ikishughulikia mahitaji ya Waandaaji kupitia uundaji wa programu ambayo itasaidia jumuiya za Wikimedia kualika washiriki wapya kwa shughuli na programu zinazoshughulikia mapungufu muhimu ya maarifa kupitia Mkakati wa Harakati Mapendekezo ya Mada zenye tija.

Lengo letu ni kuunda programu ya kusaidia waandaaji wa kampeni na hafla ili waweze kushirikisha washiriki ipasavyo kama wahariri wazuri na kuwafanya wanachama wa kudumu kama wachangiaji kwenye miradi ya Wikimedia. Programu yetu italenga zana za ujenzi ambazo husaidia waandaaji kuleta washiriki kutoka kwa ugunduzi na usajili wa matukio kupitia ushiriki wa matukio hadi mwaliko wa shughuli za siku zijazo katika harakati za Wikimedia.

Tunajua kwamba Waandalizi wa Harakati wanahitaji kuwa na uwezo wa kualika, kuratibu na kuunga mkono wahariri wapya na wa aina mbalimbali wanaojiunga na Harakati za Wikimedia na kujaza mapengo ya maarifa kwenye majukwaa (angalia Utafiti wa Waandaaji wa Harakati). Kwa kiasi kikubwa katika histroia ya Wikimedia, kampeni na matukio ya kuhariri kwenye majukwaa kama Wikipedia au Commons yameegemea mchanganyiko mifumo tata ya kijamii na zana zinazosimamiwa na watu wa kujitolea au washirika ambazo hazijaunganishwa kikamilifu kwenye programu ya MediaWiki. Hata hivyo, msuluhu hizi za zana huwa hazikui au kushughulikia mahitaji katika miktadha mipya kwa kadri inavyoibuka, na hivyo kuunda vizuizi kwa waandaaji wapya na wenye uzoefu, hasa harakati inapoangazia Usawa wa Maarifa.

Timu ya bidhaa ya WMF hushirikiana na uwekezaji wa jamii katika shirika la Wikimedia kupitia utoaji wa ruzuku, ukuzaji uwezo na ubia. Ili kuelewa michakato tata inayohusika katika kuandaa kampeni, tunapendekeza waraka wa utendakazi wa mratibu. Ili kusaidia mahitaji haya mengine tunafanya kazi na timu ya programu za Kampeni.

Watu

Mipango na maono ya timu

Kama timu, maono yetu ni kujenga msaada thabiti na wa muda mrefu kwa matukio ya kampeni za Wikimedia. Ili kuwezesha hili, tunapanga kuunda jukwaa la Matukio ya Kampeni. Jukwaa hili litakuwa na muandaji wa tukio na upande wa mshiriki wa tukio. Upande wa waandaaji utatoa zana na nyenzo ambazo waandaaji wanahitaji ili kuunda na kusimamia matukio ya kampeni yenye tija kwa jamii. Upande wa mshiriki utatoa mwongozo na usaidizi ambao washiriki wanahitaji ili kushiriki kikamilifu kwenye kampeni za Wikimedia. Kumbuka kuwa maelezo ya jukwaa hili bado yanabainishwa.

Kwa ujumla, jukwaa hili litakuwa:

  • Unaweza kugawanyika: Hii ina maana kwamba vipengele vinaweza kutenganishwa na kuunganishwa upya, kulingana na mahitaji maalum ya wiki au jumuiya.
  • Inaweza Kupanuliwa: Hii ina maana kwamba vipengele vinaweza kuongezwa hapo baadaye na timu yetu, timu nyingine au watengenezaji wa kujitolea.

Kwa hapa mwanzoni, tutajikita katika kujenga upande wa mratibu wa jukwaa, ambalo kwa sasa tunaliita "Kituo cha Mratibu" (kumbuka: jina hili linaweza kubadilika, pamoja na majina yote ya vipengele tunavyovitaja katika hatua hii). Programu ya kwanza katika Kituo cha Mratibu itakuwa suluhisho la mpangilio wa usajili. Baada ya muda, tunapanga kushughulikia maombi ya juu ya tukio la kampeni (kama inavyofafanuliwa kwenye picha hapa chini). Tulipata orodha hii ya maombi kwa kufanya mahojiano na zaidi ya waandaaji wa matukio 50 kote katika harakati hizi za WMF, ikiwa ni pamoja na kuchimba kwa undani katika tafiti na taarifa zilizopo.

Kuhusu upande wa mshiriki wa mfumo huu, tunatambua umuhimu wake mkubwa. Kwa sababu hii, tunapanga pia kutilia mkazo kuhusu hilo baadaye, baada ya kujenga baadhi ya miundombinu ya msingi kwa upande wa muandaaji wa tukio.

Maombi makuu ya kuboresha kampeni za Wikimedia, kwa mujibu wa maoni kutoka kwa waandaaji wa kampeni

Tunaamini kuwa usajili ni msingi thabiti wa kwanza katika mfumo huu. Kwa kuufanyia kazi kwanza, tutakuwa katika nafasi nzuri ya kufanya kazi katika miradi inayofuata. Bado hatujui mpangilio ambao tutashughulikia maombi mengine, lakini tumetoa ramani hii (tazama hapa chini) ili kuonyesha baadhi ya njia tunazoweza kuchukua.

Kituo cha Muandaaji na Nyenzo za usajili kama vitu vya muhimu kwa kazi za kampeni zinazotarajiwa kufanyika hapo baadae.

Tutakuwa tukitoa taarifa mara kwa mara katika ukurasa huu kadri mchakato wetu wa mawazo kuhusu mipango na mikakati ya timu yetu unavyoendelea. Wakati huo huo, unaweza kufuatilia ukurasa wetu wa mradi au kujiandikisha kupata barua pepe zetu ili ubaki unataarifa kuhusu kinachoendelea kuhusuiana na mradi wetu.

Evidence

Harakati za WMF kwa muda mrefu zimekuwa zikiomba zana bora kwa waandaaji wa matukio. WMF imefanya kazi ya kurekebisha kwa hatua mahususi kuhusiana na mchakato wa kuripoti na utekelezaji wa matukio na kampeni (kama vile Kuboresha Notisi Kuu kwa matukio ya utangazaji au vipengele vya orodha ya Matamanio ya Teknolojia ya Jamii), au mahitaji muhimu kuhusu kuripoti na hatua nyingine za mchakato ( kama vile zana za vipimo). Hata hivyo, WMF haijawekeza kwa utaratibu suala zima la waandaaji na washiriki kwenye matukio.

Tunatumia utafiti wa huko nyuma kuhusu Waandaaji na Programu ili kusaidia timu yetu kuelewa mahitaji. Utafiti mkubwa uliofanyika ni pamoja na:

Kazi ya zilizopita zinazo husiana na kazi hii

Hapo awali kumekuwa na uwekezaji katika zana au programu ambayo ilisaidia ufanyaji wa kampeni? Tafadhali unganishe taarifa hizo hapa:

Kurasa ndogo

Subpages of Foundation Product Team