Mkataba wa Harakati/Kamati ya Uandishi/Tangazo - Rasimu ya mwisho inapatikana
Andiko la mwisho la Mkataba wa Harakati wa Wikimedia sasa liko kwenye Meta
- Unaweza kupata ujumbe huu ukiwa umetafsiriwa katika lugha za ziada kwenye Meta-wiki. Please help translate to your language
Habarini nyote,
Andiko la mwisho la Mkataba wa Harakati wa Wikimedia sasa linapatikana kwenye Meta katika zaidi ya lugha 20 kwaajili ya kujisomea.
Mkataba wa Harakati wa Wikimedia ni nini?
Mkataba wa Harakati wa Wikimedia ni waraka uliopendekezwa kufafanua majukumu na wajibu kwa wanachama na vyombo vyote vya harakati za Wikimedia, ikijumuisha kuundwa kwa chombo kipya - Baraza la Kimataifa - kwa ajili ya utawala wa harakati.
Jiunge na "Tafrija ya Kuzindua" Mkataba wa Harakati wa Wikimedia
Jiunge na “Tafrija ya Uzinduzi” mnamo Juni 20, 2024 saa 14.00-15.00 UTC (kwa saa eneo unalotokea). Wakati wa wito huu, tutasherehekea kuzinduliwa kwa rasimu ya mwisho ya Mkataba na kuwasilisha maudhui ya Mkataba. Jiunge na ujifunze kuhusu Mkataba kabla ya kupiga kura yako.
'Kura ya uidhinishaji wa Mkataba wa Harakati
Upigaji kura utaanza kwenye SecurePoll mnamo Juni 25, 2024 saa 00:01 UTC na utakamilika mnamoJulai 9, 2024 saa 23:59 UTC. Unaweza kusoma zaidi kuhusu mchakato wa kupiga kura, vigezo vya kustahiki, na maelezo mengine kwenye Meta.
Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali acha maoni kwenye Ukurasa wa Majadiliano wa Meta au tuma barua pepe kwa MCDC kwenda mcdc@wikimedia.org.
Kwa niaba ya MCDC,