Strategy/Wikimedia Foundation/2015/Community consultation/Background/sw

This page is a translated version of the page Strategy/Wikimedia Foundation/2015/Community consultation/Background and the translation is 86% complete.

Usuli

Ndani ya WMF hivi majuzi tumeanzisha mpango wa kusasisha mwelekeo wetu wa mikakati ili kuhakikisha kwamba tunaendelea kufanya kazi kwa njia bora zaidi ili kutimiza ruwaza ya Wikimedia.

Kama unavyofahamu, katika mwaka wa 2009, Wakfu wa Wikimedia ulibuni mkakati wa miaka mitano kwa harakati ya Wikimedia kwa mchango mkubwa wa jamii na wafanyakazi. Kutokana na hilo, malengo ya miaka mitano yaliwekwa. Malengo hayo yalivutia uwekezaji katika kuimarisha miundombinu yetu ya kiufundi, kuunda nafasi ya uvumbuzi, na kuongeza uwekezaji katika zana za kuhariri. Mpango huo ulikuwa wa ujasiri na kutia moyo, lakini kilele cha muda wa miaka mitano ulionekana kuwa mgumu kuukabiliana na hali ya wavuti inayobadilika.


Mpango wa Kimkakati wa mwaka wa 2009 ulikuwa mpana sana na wenye mambo mengi. Ulionyesha masuala makuu kwa Harakati ya Wikimedia na mamilioni ya watu ambao ni sehemu yake. Katika mazoea, WMF ilikuwa na ugumu kuangazia na kupea kipaumbele shughuli zake za kila siku kuhusiana na Mpango huo. Tangazo la "Kupunguza Lengo" la mwaka wa 2012 lilikuwa jaribio la kupunguza lengo la WMF ili liwe lenye ufanisi zaidi katika kuunga mkono Harakati. Sasa ni wakati wa kuzingatia tena na kusasisha Mpango wa mkakati na uamuzi wa Kupunguza Lengo.


Kuelekea mwaka wa 2015, WMF inaunda mchakato mpya wa mkakati. Badala ya kujaribu kubuni hati ya miaka mitano kwa harakati nzima, tunaanzisha kitakachokuwa kanuni ya uchunguzi, tathmini na uainishaji endelevu wa mkakati. Mchakato huu wenye ufanisi zaidi unaoweza kutumika zaidi utafahamisha na kusasisha moja kwa moja vipaumbele na malengo yetu na kutusaidia kudumisha mwelekeo wa kimkakati ambao ni imara na ruwaza ya Wikimedia, unaunga mkono miradi ya Wikimedia, na unafahamu zaidi mazingira yanayobadilika ya kimataifa.


Ushauri wa Kijamii wa “Ruwaza ya Kimkakati” ndiyo hatua ya kwanza katika mchakato wetu wa kimkakati. Ni fursa kwetu kuchunguza pamoja kilichoko kwenye siku za usoni kwa Harakati na miradi ya Wikimedia. Tutajifunza kutoka kwa dhana zako na kuzitumia kufahamisha na kuboresha fikra zetu za mkakati. Kutokana na hilo, tutafafanua Mwelekeo wa Mkakati wa WMF, ambao tutashiriki nawe katika mwaka wa 2015. Mwelekeo huu wa Mkakati utatuongoza katika kuungwa mkono, uhandisi, ufadhili, na uchangishaji pesa wetu wa kijamii na utasasishwa kila mwaka. Pia tunaweza kuuliza maswali mahususi (kwa mfano, yanayohusiana na teknolojia au ufadhili) ambayo pia yatasaidia kuunga mkono upangaji wetu wa mkakati.