Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili/Kamati ya Uratibu/Uchaguzi/2024/Tangazo- Vigezo vya Mpiga kura

Outdated translations are marked like this.
Universal Code of Conduct

Wahariri

Unaweza kupiga kura kwa kutumia akaunti yoyote iliyosajiliwa unayomiliki kwenye Wikimedia wiki. Unaweza kupiga kura mara moja tu, bila kujali ni akaunti ngapi unazomiliki. Ili uwe na vigezo, akaunti hii moja lazima:

  • iwe haijazuiliwa kwa mapana katika zaidi ya mradi mmoja wa umma;

na usiwe bot;

  • na uwe umefanya angalau mabadiliko 300 kabla ya tarehe 17 Machi 2024 katika tovuti za wiki za Wikimedia;
  • na uwe umefanya angalau mabadiliko 20 kati ya 17 Machi 2023 na 17 Machi 2024.

Zana ya kuchunguzia ustahiki wa akaunti inaweza kutumika kuthibitisha kwa haraka ustahiki misógino wa kupiga kura wa mhariri.

Wasanidi-programu

Wasanidi programu watakuwa na sifa za kupiga kura ikiwa:

  • ni wasimamizi wa seva za Wikimedia walio na ufikiaji wa sehemu ya nje
  • au uwe umefanya angalau mojawapo ya majitoleo yaliyounganishwa kwenye repos rasmi zozote za Wikimedia, kati ya 17 Machi 2023 na 17 Machi 2024.

Kigezo cha ziada

  • au uwe na moja ya majitoleo yaliyounganishwa kwenye repo yoyote kwa nonwmf-extensions au nonwmf-skins, kati ya 17 Machi 2023 na 17 Machi 2024.
  • au uwe umejitolea angalau mchango mmoja uliounganishwa kwenye repo yoyote ya zana za Wikimedia (kwa mfano magnustools) kati ya 17 Machi 2023 na 17 Machi 2024.
  • au uwe mmoja wa watunzaji/wachangiaji wa zana, roboti, vifaa na moduli zozote za Lua kwenye Wikimedia wiki.
  • au uwe umejihusisha kwa kiasi kikubwa katika kubuni na/au kukagua michakato ya maendeleo ya kiufundi inayohusiana na Wikimedia.

Watafsiri

Watafsiri watakuwa na sifa za kupiga kura ikiwa wamefanya angalau mabadiliko 300 kabla ya tarehe 17 Machi 2024, na mabadiliko 20 kati ya 17 Machi 2023 na 17 Machi 2024, kwenye translatewiki.net.

Wafanyakazi na wakandarasi wa Wikimedia Foundation

Wafanyakazi wa sasa wa Wikimedia Foundation na wanakandarasi watakuwa na sifa za kupiga kura ikiwa wameajiriwa na Shirika kufikia tarehe 17 Machi 2024.

Wafanyakazi na wakandarasi wa washirika wa Wikimedia

  • Chapta za sasa za Wikimedia, shirika la kimada au wafanyakazi wa kikundi cha watumiaji na wanakandarasi watakuwa na sifa za kupiga kura ikiwa wameajiriwa na shirika lao kufikia tarehe 17 Machi 2024.
  • Wanachama wa mashirika rasmi kama inavyofafanuliwa katika sheria ndogo za sasa za Chapta za Wikimedia, mashirika ya mada au vikundi vya watumiaji watakuwa na sifa za kupiga kura ikiwa wamekuwa wakihudumu katika shughuli hizo hadi tarehe 17 Machi 2024.

Kamati ya Ushirikiano na Kamati ya Uchaguzi itathibitisha orodha ya Washirika wa Wikimedia wanaostahiki kufikia wakati wa mwito wa wagombea.

Wajumbe na washauri wa bodi ya Wikimedia Foundation

Wanachama wa sasa wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Wikimedia Foundation, wanachama wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Wikimedia Foundation na washauri wa kujitolea kwa kamati za Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Wikimedia Foundation wanastahiki kupiga kura.

Wanachama wa kamati za harakati za Wikimedia

Wanachama wa sasa wa kamati za harakati za Wikimedia wanastahiki kupiga kura ikiwa wamekuwa wakihudumu katika shughuli hizo kuanzia tarehe 17 Machi 2024.

Kamati ya Uchaguzi itachapisha orodha ya kamati zinazostahiki za vuguvugu la Wikimedia kwa madhumuni ya sehemu hii kufikia wakati wa mwito wa wagombea.

Waandaaji wa jumuiya ya harakati za Wikimedia

Waratibu wa jumuiya walio na hadhi nzuri, ambao hawana sifa ya kupiga kura kwenye kategoria nyingine, wanahitimu kupiga kura iwapo watakutana na mojawapo ya yafuatayo:

  • wametuma maombi, kupokea na kuripoti angalau moja ya ruzuku zaWikimedia Foundation tangu tarehe 17 Machi 2024.
  • walikuwa waandaaji wa angalau tukio moja la hackathon lililofadhiliwa, shindano au tukio lingine la Wikimedia lililo na hati za Wiki na angalau wahudhuriaji/wageni/washiriki 10 kati ya tarehe 17 Machi 2023 na 17 Machi 2024.

Vidokezo

Ikiwa unakidhi vigezo vikuu, utaweza kupiga kura mara moja. Kwa sababu ya vikwazo vya kiufundi vya SecurePoll, watu wanaotimiza vigezo vya ziada huenda wasiweze kupiga kura moja kwa moja, isipokuwa pale watakapotimiza vigezo vingine. Iwapo unaona kuwa unakidhi vigezo vya ziada, tafadhali tuma barua pepe kwa board-elections@lists.wikimedia.org yenye hoja angalau siku nne (4) kabla ya tarehe ya mwisho ya kupiga kura, yaani, tarehe 21 Aprili 2024 au kabla yake. Ukitimiza vigezo, tutakuongeza kwenye orodha ya kwa mkono, ili uweze kupiga kura.