Jenga Wikipedia ya Kiswahili

Jenga Wikipedia ya Kiswahili
Logo of Jenga Wikipedia ya Kiswahili

Utangulizi - Introduction

edit
Jenga Wikipedia ya Kiswahili ni kundi la wahariri na wakabidhi wa Wikipedia ya Kiswahili waliowahi kushiriki katika kazi hii tangu miaka 10 hivi ilhali wanakaa katika nchi mbalimbali. Wikipedia ya Kiswahili ni kamusi elezo la pekee kwa lugha hii hivyo ina nafasi na wajibu wa kukua na kuwa chanzo muhimu cha elimu kwa wasemaji wote wa Kiswahili. Jenga Wikipedia ya Kiswahili (« Build Swahili WIkipedia ») is a group of editors and admins at this Wikipedia who have cooperated for about 10 years while living in different countries. Swahili Wikipedia is the only encyclopedic resource in this language and thus has the chance and responsibility to grow and be an important source of knowledge for all speakers of Swahili.

Shabaha - Objectives

edit
Tunalenga kuimarisha Wikipedia ya Kiswahili na kuiboresha.
  • Tunahitaji kupanusha mada za makala na kuhakikisha kiwango cha ubora.
  • Tunalenga kupanusha idadi na uwezo wa wahariri na hasa wahariri wenyeji wa Afrika ya Mashariki.
  • Tunalenga kujenga sifa za Wikipedia katika jamii na taasisi za elimu.
We aim to strengthen Swahili Wikipedia and make it better.
  • We need to widen the topics we write on and work on article quality
  • We strive to involve more editors and help to build their abilities, and especially get more contributors from East Africa
  • We aim to strengthen the awareness of Wikipedia and its image in society and educational institutions.

Shughuli - Activities

edit
  • Tunaendelea kushauriana kwa njia ya intaneti
  • wengine wetu tunaendelea kushauriana moja kwa moja na wahariri wapya huko Morogoro na Dar es Salaam
  • Tunatarajia kuongeza warsha kwa ajili ya wanavyuo katika Afrika ya Mashariki
  • Baada ya muda fulani itakuwa vema kupata tena nafasi ya mkutano wa wahariri
  • We keep on consulting online
  • several of our members are directly involved in coaching new editors in Morogoro and Dar es Salaam
  • We plan to have more workshops for people at universities in East Africa
  • after some time it will be good to bring our group together again for a meetup


Historia - History

edit
Katika miaka 10 tangu kuingia katika Wikipedia ya Kiswahili tulishauriana kupitia intaneti ilhali tulikaa Tanzania, Kenya, Ujerumani na Uajemi.
  • Mwaka 2015 tulikutana mara ya kwanza ana kwa ana kwa msaada wa WMF tukifanya warsha kwa walimu na wanafunzi wa shule moja mjini Morogoro, Tanzania. Mkutano huu ulikuwa muhimu kwa maelewano na kushikamana katika kundi letu.
  • Tangu warsha ile kuna klabu ya Wikipedia ambako wanafunzi wanaendelea kuchangia katika Wikipedia, walisaidiwa na mmoja wa kundi letu anayefanya kazi katika shule hii
  • Mwaka 2017 tuliendesha warsha kwa ajili kundi la wanafunzi wa vyuo mbalimbali mjini Dar es Salaam. Tokeo lake ni kundi la wahariri wapya.
  • Tuliweza kujenga uhusiano na Shirika la Astronomia Tanzania na Idara ya Kiswahili kwenye Chuo Kikuu ambako wahusika walivutwa na nafasi ya kusambaza elimu ya kisayansi kwa njia ya Wikipedia
  • Mwaka 2018 tulikuwa na warsha ya kuandaa "Kamusi ya Astronomia" tuliyoendesha pamoja na ASSAT (Astronomy and Space Science Association of Tanzania) na washiriki kutoka Taasisi ya Taaluma ya Kiswahili (Chuo kikuu cha Dar es Salaam)
In the 10 years since we joined Swahili Wikipedia we communicated via the internet while living in Tanzania, Kenya, Germany and Iran
  • In 2015 we had a first direct meeting with financial assistance from WMF, in combination with a workshop for teachers and students of a Secondary School at Morogoro, Tanzania. This conference was important for our mutual understanding and motivation
  • Since that workshop a Wikipedia club has been in existence at that secondary school and is being looked after by one of our members working at that school
  • In 2017 two of our members could run a series of workshops and editathons for university students at Dar es Salaam. The result is a group of new editors who keep on contributing. (it became Wikimedia User Group Tanzania)
  • We could make contact with several academic institutions at Dar and introduce Wikipedia there

Mawasiliano nasi - Contact information

edit

Users Kipala and Muddyb

Wanaopenda kushiriki - Interested in participating

edit

Kama umeshashiriki hapa na kuchangia kwa muda wa angalau mwaka moja unakaribishwa kujiunga nasi. Peleka ombi lako kwa Muddyb, Kipala au andika kwenye ukurasa wa majadiliano!

Kurasa za ziada

edit

Mipango endelevu (ongoing plans)

edit