Wikimedia Community User Group Linguila

This page is a translated version of the page WikiLinguila and the translation is 83% complete.
Outdated translations are marked like this.

WikiLinguila Community User Group au WikiLinguila (Wikimedia kwa lugha za wachache za Afrika ya Kati) ni kikundi cha watumiaji walio jitolea kukuza kazi ya Wikimedia katika lugha ya Kibantu ya eneo la Afrika ya Kati, kwa kuchukua lugha za Kikongo na Lingala kama mifano. Hizo lugha za Kibantu zinatumika katika Afrika ya Kati, wakiwemo wasemaji milioni 26 wanaoziona kama lugha mama (Lingala milioni 20 na Kikongo milioni 6) mbali na idadi isiyojulikana ya wasemaji waliosambaa sehemu mbalimbali, kwa kuunda kundi la lahaja za lugha rasmi katika nchi tatu za eneo hilo, yaani: Kongo-Kinshasa, Kongo-Brazzaville na Angola, mbali na idadi ndogo zaidi kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Gabon na Sudan Kusini.

Kikundi cha Watumiaji Wikimedia wa Taifa Linguila
LocationAfrika ya Kati :
Congo-Kinshasa
Congo-Brazzaville
Angola
Official language(s)Kingala, Kikoongo
Other language(s)Kiteke-Ibali, Kiluba-Kasai, Kiswahili, Kitetela, Kiluba-Katanga, Kituba, Kibangi, Kihunde
Websitewikilinguila.org

Langila ni lugha ya Kilingala katika umbo lake la kimisimu. Ni lugha inayozungumzwa na watu wanayofahamiana. Pia wanatumia neno hilo kubainisha aina zote za lugha zinazozungumuzwa duniani, hivyo WikiLangila kama Wiki ya lugha mojawapo au Linguila kama Wiki ya kilugha kama jumuia ya wanaisimu na wasemaji wa lugha za Afrika ya Kati.

Mradi huu unatia moyo na kusaidia pia jumuia nyingine za Afrika ya Kati, ambapo vuguvugu hili halijaanza na halina wanachama hadi sasa. Lengo ni kuchangia miradi ya Wikimedia. Kimsingi, ingekuwa vizuri kuwa na makundi tofauti ya watumiaji, kwa mfano, wa Lingala Wikimedians User Group na Kikongo Wikimedians User Group, lakini unganishaji wa lugha hizo zenye uhusiano mkubwa za eneo maalumu sana la bara unaweza kuleta faida sana. Kuhusu lugha za Téké na Luba-kasaï zinazozungumuzwa katika Afrika ya Kati, ndani ya Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Gabon. Kwa lugha za Téké na lugha ya Luba-Kasaï za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kaskazini mwa Angola tunapanga kuendelea kidogokidogo.

Kwa sasa shida kubwa zaidi ni kupata katika maeneo hayo watumiaji wa Wikimedia au watu wenye kuvutiwa na mradi huo. Sisi tunaalika yeyote yule anayeishi katika maeneo hayo aisaidie dunia kugundua lugha zetu, zinazoelekea kusahaulika. Wazungumzaji wengi wanaweza wasijue umuhimu wa kuchangia maudhui kwa lugha za kienyeji na wanaweza kukosa ujuzi wa kufanya hivyo kwa ufanisi.

WikiLinguila inalenga kukuza uonekano na kuendeleza maudhui ya kidijiti ya lugha za taifa za nchi za eneo la Afrika ya Kati, kama njia nzuri ya kudumisha kwa wakati huohuo urithi wa utamaduni wa makabila madogo kupitia miradi ya Wikipedia na miundo mingine inayojitahidi kufanya utamaduni wao upatikane katika mtandao. Dhima yetu hasa ni kukuza, kuhamasisha na kutokeza wazi maudhui yaliyoundwa katika lugha zetu za taifa, ili mradi huo uwe wetu wenyewe, kwa sababu unatusaidia kutetea utambulisho wetu kama watu na wasemaji wa eneo la Afrika ya Kati. Kwa kufanya hivyo, tunahakikisha kwamba pamoja dunia inakuwa ndogo zaidi katika kuwasiliana na kufanya mambo tele ya kujenga.

Uanachama

Uanachama wa kikundi hiki uko wazi kwa yeyote anayevutiwa.  

Kwa mawasiliano