Mpango wa Mwaka wa Wikimedia Foundation/2023-2024/Bidhaa & Teknolojia/Malengo na Matokeo Muhimu(OKRs)

This page is a translated version of the page Wikimedia Foundation Annual Plan/2023-2024/Product & Technology/OKRs and the translation is 99% complete.
Outdated translations are marked like this.
Kumbuka – Tafsiri za ukurasa huu zitaratibiwa na WMF kila baada ya miezi 3, hadi katikati ya 2024:
AR, FR, PT, RU, ES, JA, UK, ZH, SW, HI

Nyaraka hii inawakilisha "sehemu ya 2" ya mchakato wa Upangaji wa Mpango wa Mwaka wa 2023-24 kwa idara za Bidhaa na Teknolojia za Shirika la Wikimedia Foundation. Inaangazia rasimu ya idara' kuhusu "malengo na matokeo muhimu" (OKRs) ya Mpango wa Mwaka wa 2023-24. Wikimedia Foundation Annual Plan/2023-2024/Product & Technology"Sehemu ya 1" ilikuwa maelezo ya majalada ya rasimu za kazi (zinazoitwa "ndoo") na nadharia na mipango iliyo nyuma ya hati hii.

Ingawa waraka huu umekamilika, inakusudiwa kuwa Matokeo Muhimu, na dhana zake za kimsingi, zitasasishwa mara kwa mara katika Mpango wote wa Mwaka wa 2023-24 kadri ya yale tutakayojifunza.

Ndoo ya 1: Matukio ya Wiki

Malengo v2 (v1) Matokeo Muhimu Maelezo

WE1: Uzoefu wa mchangiaji

Kusaidia ukuaji wa ubora wa maudhui kwa ubora wa hali ya juu na kuwa na maudhui yanayohitajika ndani ya mfumo wa kiulimwengu wa ikolojia ya elimu ya bure wenye lugha nyingi tofauti, unaoaminika na mpana zaidi kwa kuwezesha na kuunga mkono uzoefu wenye ubora wa hali ya juu na unaofikiwa.

Muktadha: Ili kulipa kipaumbele jambo mojawapo tunahitaji kubadilishana na lingine. Tunataka kujikita katika kusaidia maudhui na wasimamizi wa maudhui, michango kupitia simu za mkononi, kusaidia kampeni za mtandaoni, na kupunguza vizuizi vya ufungiaji wa anwani za IP. Ili kuangazia mambo hayo inabidi kupunguza kipaumbele katika msaada kwa tukio la ana kwa ana na ufanisi wa mhariri mpya (isipokuwa kitengo cha Matokeo Muhimu cha ufungiaji wa anwani za IP).

Jadili

1. Kuongeza michango ya simu isiyorekebishwa kurudi kwenye toleo lililotangulia katika maeneo makuu ya wiki ya makala kwenye Wikipedia kwa 10%, wastani uliopatikana kupitia seti wakilishi ya miradi mbalimbali ya wiki. Matokeo Muhimu (KR) haya yanatoa uhimizo mpana wa kukuza uhariri wa maudhui kupitia simu, kupitia shughuli zinazosaidia Matokeo Muhimu mengine (k.m. udhibiti na utangazaji wa maudhui) na kupitia shughuli zinazolenga hasa mchango wa simu za mkononi. Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, mchango wa maudhui ya mtandao wa simu umeongezeka kwa takriban 20%. Ikiwa tunaweza kuja na njia za kuiongeza kwa 10% zaidi katika mwaka mmoja tu, hiyo itakuwa kasi zaidi ya kiwango chake cha asili cha ongezeko.

KR hii inajumuisha wavuti na programu. Imepatikana kwa kuchukua "wastani wa seti ya uwakilishi wa wiki mbalimbali" ili kuhakikisha kwamba tunafanya maboresho ambayo ni muhimu kwa wiki nyingi, na sio tu zile kubwa zaidi. Tutachagua ni miradi ipi ya wiki hapo baadaye.

2. Kukamilisha uboreshaji wa mitiririko minne ya kazi nne ambayo huboresha uzoefu wa wahariri na haki zilizopanuliwa (wakabidhi, walinda doria, watendaji, na wasimamizi wa kila aina); kupanua ubunifu wao; itaathiri angalau miradi ya wiki minne tofauti, na kukutana na KR kwa kila uboreshaji uliowekwa kwa ushirikiano na watu wanaojitolea. Bado hatujui kama lengo mahususi la, tuseme, kama ni kupunguza mzigo, ama kimsingi, ni kile ambacho wahariri hawa wanaofanya kazi ya usimamizi wanahitaji kutoka kwetu. Hatimaye, tunataka kutumia rasilimali zetu ili kuongeza kuridhika kwao na kuongeza uwezo wao wa kujenga na kudhibiti mtiririko wa kazi -- hiyo ndiyo maana ya "kuongeza ubunifu wao": wanajamii hawa wameunda vitu vya kustaajabisha, na baadhi ya njia bora zaidi tunaweza kusaidia. ni wakati tunawasha ubunifu huo kupitia mifumo, vidokezo, vigezo na zana zingine. Nambari ya "mifumo minne ya kazi" ni kwa sababu ya timu ngapi tunaweza kufikiria kufanyia kazi KR hii. Na idadi ya "wiki nne tofauti" ni ya kutuhimiza kujumlisha athari zetu katika miradi yote inapowezekana. KR hii itatuhitaji kufanya kazi na watu walioathiriwa wa kujitolea kuweka KR halisi kwa kila uboreshaji, ili tuweze kukubaliana nao kuhusu ni muda gani tunakuwa tumepata athari. Kumbuka kuwa kazi ya utiririshaji kazi inayotumiwa na watumiaji wengine isipokuwa wahariri wanaofanya ukaguzi bado inaweza kuboresha uzoefu wao. Kwa mfano, kazi ambayo husababisha wachangiahi wapya kuunda makala ya kwanza yenye nguvu zaidi inaweza kuboresha mizigo ya wale wanaoshika doria katika makala mpya.
3.Ongezeko la asilimia 1 mwaka baada ya mwaka(YoY) katika sehemu ya makala mpya au zilizoboreshwa kuhusu mada zenye athari kubwa na ubora unaokubalika, kulingana na "alama ya ubora wa kimataifa", ambayo huundwa au kuhaririwa kwenye Wikipedia, kwa kuanzia na maeneo ya kijiografia yenye uwakilishi mdogo na jinsia. Tunapopata maelezo zaidi na kuweka misingi, kipimo hiki kinaweza kurekebishwa ikiwa ni pamoja na kubadilika ili kuhalalisha na/au kurekebishwa ili kufidia mabadiliko mbalimbali. Kipimo hiki kinaangazia ongezeko la maudhui yenye ubora unaokubalika kwa mada zenye athari kubwa. Hasa, lengo ni kuwa na ziada ya 1% ya makala zenye ubora unaokubalika kwenye mada zilizochaguliwa (kuanzia na maeneo ya kijiografia na jinsia) kwenye Wikipedia, ikichukua mwaka uliopita kama msingi. Kwa mfano, kati ya makala zote mpya au zilizoboreshwa mwaka 2022/2023 ambazo zilikuwa zinahusu maeneo ya kijiografia na zilizotimiza alama za ubora unaokubalika, 28% zililenga maeneo yenye uwakilishi mdogo. Hii ina maana kwamba, kwa mwaka 2023/2024, kati ya makala zote mpya au zilizoboreshwa kuhusu maeneo ya kijiografia ambazo zinafikia alama ya ubora unaokubalika, 29% zinapaswa kuzingatia maeneo yenye uwakilishi mdogo wa kijiografia. Kumbuka kuwa lengo limebadilika kutoka ukuaji wa 10% wa mwaka baada ya mwaka (kama ilivyoandikwa hapo awali) hadi ukuaji wa 1% wa mwaka baada ya mwaka. Kipimo hiki kilibadilishwa hadi 1% mwaka baada ya mwaka(YoY) kwa sababu kilibainishwa kuwa kinaweza kufikiwa zaidi na cha uhalisia na wachanganuzi wa data katika Shirika la Wikimedia Foundation, kutokana na mitindo ya hivi majuzi ya ukuaji wa makala kuhusu mada zenye athari kubwa (pamoja na mwonekano mahususi wa maudhui kwenye maeneo yenye uwakilishi mdogo katika Wikipedia).

Kipimo hiki kimekusudiwa kuwa muhimu kuweka mwelekeo lakini rahisi kwa timu kufafanua mkakati wao na kufuatilia maendeleo. Juhudi za kufikia lengo hili zinaweza kulenga kuboresha ubora wa makala zilizopo kwenye mada zilizochaguliwa au kuhimiza kuundwa kwa makala mpya kuhusu mada hizo. Timu zinaweza kutathmini matokeo yao kwa kulinganisha matokeo ya robo au mwaka mzima na kipindi kama hicho mwaka mmoja kabla. Vipengele kama vile ubora na umuhimu daima ni vigumu kupima. Ubora wa makala hubainishwa na alama ya ubora duniani, ambayo inategemea vigezo vingi vya makala, kama vile idadi ya sehemu, marejeleo na viungo. Vile vile, mada za makala zitatambuliwa kwa ushirikiano na timu zinazoshughulikia uchanganuzi wa pengo la maarifa na zitatumia seti za data, kwa kuanza na maeneo yenye uwakilishi mdogo wa kijiografia na jinsia.

Kazi hii inaendana na kipimo cha Shirika cha maudhui kwa upana wake , huku kikigusa vyote uwingi na ubora - hii inamaanisha kuwa tunaweza kuvifanikisha hivyo vyote kwa kuanzisha makala mpya au kwa kuboresha zilizopo. "Mada zenye athari kubwa" ni dhana kutoka Pendekezo la Mkakati wa Harakati #8: "Kutambua Mada zenye Athari". Jinsia na jiografia zote ni mada ambazo harakati zetu zimeangazia kuwa zina mapungufu muhimu ya maudhui na ambazo timu yetu ya Utafiti ina vifaa vya kupima.

4. Ongezeko la X% la kiasi cha vizuizi vya anwani za IP ambavyo hukatiwa rufaa, kukiwa na mgao tuli au unaopungua wa rufaa ambazo zinafunguliwa. Vizuizi vya anwani za IP ndio zana kuu ya harakati zetu ya kukomesha watumiaji wabaya wa tovuti zetu, lakini ina athari mbaya ya kuzuia watumiaji wengi ambao wanafanya kwa nia njema. Hii husababisha athari mbaya haswa kwa wahariri wapya na kwenye programu za jumuiya. Hakuna njia ya kuaminika ya kupima ni watu wangapi wamezuiwa kimakosa, lakini tunaweza kukadiria kupitia ni wangapi kati yao wanaomba msamaha (yaani rufaa) baada ya kuzuiwa. Kikwazo cha kufanya hivi, ingawa, ni kwamba mchakato wetu wa kukata rufaa ni mgumu kwa watumiaji kuupata na kuukamilisha. Kwa hivyo, KR hii inajaribu kutuongoza kuboresha hali ya uzuiaji wa anwani za IP kwa pande mbili. Kwanza, inatutaka tufanye mchakato wa kukata rufaa uwe wazi kwa watumiaji, ili kwamba tutegemee kuona watu wengi waliozuiwa wakikata rufaa. Na wakati huo huo inatutaka kupunguza idadi ya vizuizi vya kimakosa vinavyotokea tangu mwanzo kabisa kwa kuangalia uwiano wa rufaa ambazo zinafunguliwa baada ya kuwa zilifungwa hapo awali. Kwa maneno mengine, ikiwa tunaweza kuzuia watumiaji wanaostahili kuzuiwa tu, basi tutaona wachache sana wakifunguliwa. KR hii inaweza kuchochea majadiliano ya kina ya jumuiya na kiufundi kuhusu asili ya anwani za IP na jinsi tunavyozitumia, na kuhusu mzigo wa kazi na utendakazi wa watendaji wanaodhibiti michakato hii. Tunapofanya kazi na wanajamii, tunaweza kugundua kuwa kuna njia bora za kupima maendeleo kwenye masuala ya kuzuia IP, na tunaweza kuangazia tena vipimo vingine. [Angalia ujumbe wa sasisho]
5. Kuwezesha jumuiya mpya ya Wikimedia kwa ajili ya kujenga maktaba wazi ya vitendaji, Wikifunctions, ambavyo vina uwezo wa kuunda aina mpya za maarifa kwenye tovuti za Wikimedia. KR hii inanasa dau la kimkakati la Shirika juu ya kuunda Wikifunctions kama jukwaa la jumuiya kujenga, kutumia, na kudumisha maktaba ya vitendaji. Wikifunctions pia itaunda msingi wa kiufundi wa Muhtasari wa Wikipedia, mradi wa kuwezesha uundaji na matengenezo ya makala za Wikipedia kwa njia inayojitegemea kwa misingi ya lugha. Kusudi kuu Abstract Wikipedia ni kufanya maarifa kufikiwa zaidi na kutumika na kila mtu, bila kujali lugha yao au asili.

WE2: Usomaji na uzoefu wa media

Kuzalisha uzoefu wa kisasa, usomaji unaohitajika na unaoweza kufikiwa na uzoefu wa media kwaajili ya miradi yetu.

Muktadha: Tunataka kuweka mkazo zaidi katika kuongeza vifaa vya kipekee, kuongeza ugunduzi wa ndani na ushiriki nje ya kuhariri. Ili kutekeleza hayo, ni lazima tuondoe kipaumbele kwa shughuli za kujihusisha na picha na audio na masuala ya ndani yenye ufikivu. KR zilizopo hapa chini zinaonyesha mwelekeo huo pia.

Jadili

1. Kuhakikisha matumizi bora ya usomaji kwa watumiaji wote kwa kurekebisha hali ya utumiaji wa chaguomsingi kwa 15% ya idadi ambayo kurasa zimetazamwa, kulingana na mahitaji ya kibinafsi na vigezo vya mtumiaji. KR hii inalenga kuruhusu fursa ya kiolesura chetu kuendana na mahitaji ya mtu binafsi inapobidi. Dhana hapa ni kwamba watu watajisikia kujihusisha zaidi na tovuti na kiolesura ambacho kinaweza kubadilika kulingana na mahitaji yao. Hii inaweza kujumuisha kufanya kazi katika hali ya giza, msongamano wa maandishi na ukurasa, na uwekaji wa mapendeleo wa ukubwa wa maandishi. Baadhi ya urekebishaji huu unaweza kufanywa kiotomatiki na kiolesura - kwa mfano, kuunda matoleo sikivu ya kipengele au zana, au kuhakikisha kuwa hali ya giza inawashwa kulingana na kivinjari au mipangilio ya kifaa cha mtumiaji. Katika hali nyingine, urekebishaji huu unaweza kufanywa kupitia ubinafsishaji wa kimakusudi - kuruhusu watumiaji kuchagua hali zisizo chaguo-msingi katika hali mahususi (lakini ndogo). Kwa mtazamo wa ufikivu, itazingatia vipengele vinavyohitaji kujengwa kwa kujitegemea ili kuruhusu ufikivu zaidi, au kuruhusu kuweka chaguo-msingi ambazo zinafaa zaidi kwa ufikivu, huku ikiacha fursa ya kubinafsisha watumiaji ambao wana mapendeleo tofauti. Ili kuweka nambari mahususi "15%", tuliangalia jinsi watumiaji wanavyobadilisha hali ya utumiaji wa chaguomsingi katika programu ya Wikipedia iOS. 59% ya watumiaji wa programu wanatumia mandhari ambayo si chaguomsingi (ya giza, nyeusi au sepia). Tulitumia nambari hii kama msingi, lakini tulizingatia katika dhana yetu kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba watumiaji wazoefu wa Wikipedia kwenye wavuti huchukua muda kurekebisha uzoefu wao wa kusoma, tofauti na watumiaji wa hapa na pale.
2. Wasomaji wanaovutiwa watagundua na kuvinjari maudhui zaidi, yanayopimwa kupitia ongezeko la 10% la mwingiliano wa ukurasa unaorejelewa katika wiki wakilishi. KR hii inalenga kuwarahisishia wasomaji wanaovutiwa kugundua maudhui kwa kuchunguza mbinu tofauti za ugunduzi wa maudhui au sehemu za kuingia. Lengo ni kuwapa wasomaji chaguo hizi katika nyakati mahususi za safari yao au baada ya vitendo mahususi vinavyoonyesha kuwa wanapenda kujifunza zaidi. "Maingiliano ya kurasa", katika muktadha huu, ni pamoja na njia zote ambazo mtumiaji anaweza kuingiliana na maudhui zaidi ya kutazama tu ukurasa (uhakiki wa ukurasa ni mfano). "Marejeleo ya ndani" inamaanisha kuwa tutakuwa tukihesabu mwingiliano wa ukurasa unaotokea baada ya mtumiaji tayari kuanza kipindi chake kwenye mali yetu (yaani, bila kujumuisha mara ya kwanza anapotua kwenye tovuti, ambayo kwa kawaida hufanyika kupitia mapendekezo ya injini ya utafutaji).
3. Kuimarisha ushirikiano wa wasomaji na Wikipedia kupitia 0.05% ya vifaa vya kipekee vinavyohusika katika ushiriki wa usio wa kuhariri. KR hii inalenga kukuza ushirikiano wa wasomaji, huku pia ikichunguza njia ambazo wasomaji wanaweza kuchangia katika miradi yetu ambayo si kurasa za kuhariri. Tunakisia kuwa kuna watu ambao wana nia ya kujihusisha na wiki lakini ambao uhariri wa aina yoyote ni mkubwa mno kwao. Tunataka watu hao wawe na njia ya kuhusika kwa undani zaidi, labda kuwa wasomaji waliojitolea zaidi, au hatimaye kuwa na urahisi wa kuhariri. "Kushiriki bila kuhariri" kunarejelea hatua zozote ambazo watumiaji wanaweza kuchukua kwenye wiki kando na kuhariri (pia tunahesabu mabadiliko ya mijadala kama 'kuhariri'). Ingawa tovuti zetu hazina yoyote kati ya haya, programu zetu zinayo, kwa njia ya orodha za kusoma au kushirikisha maudhui kwenye mitandao ya kijamii. Kazi hii inaweza kujumuisha kuwaruhusu watumiaji kusanidi uzoefu wao wa kibinafsi wa kusoma, au inaweza pia kuzingatia kushiriki maudhui katika mradi mzima wa wiki, kuratibu, na kupendekeza maudhui kwa wengine. KR inajumuisha kazi kwenye tovuti za simu na kompyuta za mezani na programu. Kwa simu ya mkononi na kompyuta ya mezani inaweza kujumuisha utumiaji wa baadhi ya utendakazi wa ushiriki usiohariri uliopo kwenye programu. Kwa programu, inaweza kujumuisha kuboresha utendakazi uliopo au kuunda mawazo mapya. Nambari 0.05% ni takriban uwiano wa wahariri kwa vifaa vya kipekee -- kwa hivyo labda katika mwaka wa kwanza wa seti hii ya vipengele, tunaona uwiano sawa kwa washiriki wasio wahariri, ambao hatimaye utaongezeka hadi zaidi ya idadi ya wahariri hapo baadaye. [Angalia ujumbe wa sasisho]
4. Kuboresha utendakazi wa tovuti kwa watumiaji wa Amerika Kusini, kwa kuanzia na kupunguza muda wa kusubiri wa p50 kwa watumiaji nchini Brazili kwa angalau ms 100. KR hii inalenga katika kuboresha utendakazi wa tovuti katika eneo ambalo halitumiki sana. Utafiti unapendekeza kwamba kupunguzwa kwa kiasi kikubwa na dhahiri cha muda wa tovuti kutoa majibu huboresha ushiriki wa mtumiaji. Kama sehemu ya KR hii, tutaboresha muda wa tovuti kutoa majibu huko Amerika Kusini, k.m. kwa kupeleka tovuti ya ziada ya kache katika eneo hilo. Ingawa tunatarajia kuwa na athari kubwa ya kwanza inayoweza kupimika nchini Brazili kufikia mwisho wa mwaka wa fedha, eneo zima linatarajiwa kuona manufaa makubwa ya utendakazi muda mfupi baadae.

WE3: Jukwaa la Maarifa

Kuongeza ushirikiano na ufanisi miongoni mwa wasanidi programu kwa kuboresha mchakato wa usanidi wa MediaWiki

Jadili

1. Kupunguza utengano katika utendakazi wa wasanidi programu, na kufikia 75% ya kupitishwa kwa angalau zana moja ya msanidi inayotumika rasmi katika matumizi halisia. Lengo la matokeo haya muhimu ni kutoa zana za maendeleo za kawaida zinazokidhi mahitaji ya wasanidi wengi wa Wikimedia. Pia tunalenga kuweza kuiga mazingira kama ya uzalishaji kwa vipengele mbalimbali katika hatua za uundaji, majaribio na usambazaji. Kwa kukamilisha hili, tutatoa utumiaji bora zaidi wa wasanidi programu. Uzoefu huu utawaruhusu wahandisi kuingia ndani kwa haraka zaidi, kusaidiana wanapokumbana na matatizo na kupeleka vipengele vipya kwenye uzalishaji wakiwa na ujasiri zaidi. Kazi hii haikusudii kutoa utendakazi wote wa wasanidi programu katika mwaka wa kwanza, lakini kuboresha maeneo ambayo yanaathiri zaidi tija ya wasanidi programu.

2. Kuongeza kwa 20% idadi ya waandishi ambao wamejitolea zaidi ya viraka 5 kwenye seti maalum ya hazina za MediaWiki ambazo zimesimikwa tayari kwa uzalishaji.

Kuongeza idadi ya watu walio tayari na wanaoweza kuchangia mjumuisho wa msimbo wa MediaWiki kutapunguza uwezekano wa timu kuzuiwa pale ambapo mabadiliko kwenye kiini cha MediaWiki yanapohitajika. Pia hufanya uwezekano mdogo wa kuundwa suluhisho ambazo zinaongeza deni la kiufundi. Zaidi ya hayo, kipimo hiki kinaonyesha kuwa msingi wa msimbo unakuwa rahisi na salama zaidi kuchangia bila athari zisizotarajiwa.
Kutafuta uvumbuzi na kuandika vitu vikuu 4 vya mwelekeo wa kimkakati wa kiufundi/sera/mchakato. Uongozi wa Bidhaa na Teknolojia umebainisha maeneo muhimu ambayo mwelekeo wa kimkakati unahitajika ili kuongeza athari za kazi ya kiufundi. Mifano ni pamoja na kufafanua mbinu ya kutumia MediaWiki nje ya Wikimedia na kuunda sera ya programu huria. Kufafanua mwelekeo wa kimkakati wa mada hizi kutamaanisha kuongezeka kwa ufanisi na uwiano zaidi katika mwelekeo wa kiufundi wa Wikimedia.

Malengo v2 (v1) Matokeo Muhimu Maelezo

SDS1: Kufafanua vipimo muhimu

Kila kigezo na kipimo katika seti yetu ya data muhimu ya kipimo inaungwa mkono kisayansi au kimajaribio, imeboreshwa, imezalishwa na kushirikishwa kote kwenye Shirika.

Muktadha: Utumiaji mzuri wa vipimo kufanya maamuzi ya kimkakati katika Shirika kunatuhitaji kupima na kutathmini athari ya kazi kwa kutumia vipimo vya kawaida, vya kutegemewa na vinavyoeleweka vyema. Kuhakikisha kwamba timu tofauti zinazofanya kazi kwenye miradi tofauti zinatumia vipimo sawa vilivyo na ufafanuzi sawa ili kuelewa athari ya kazi yao kutaturuhusu kuoanisha juhudi kote kwenye Shirika, na washirika, na jumuiya. Vipimo hivi vitaruhusu wafanyakazi wa Shirika na jumuiya kutathmini mapendekezo ya programu na vipengele vya bidhaa na kufuatilia na kutathmini matokeo. Na huwawezesha wahandisi wanaotumia zana zinazotumika katika utayarishaji na uchanganuzi wa data kutoa huduma ya kiwango cha juu zaidi kwa kufafanua kwa usahihi zaidi upeo wa kazi yao, na kufanya juhudi kushughulikiwa zaidi na rasilimali zetu za sasa. Data ni muhimu tu kama inavyoweza kufikiwa na watumiaji. Vipimo vyetu lazima viwe na ufikiaji wa juu zaidi ili kuongeza matumizi yake kwa hadhira zote. Tutakusanya, kupanga, na kutoa taarifa muhimu ili kuongoza matumizi sahihi na kuzuia matumizi mabaya.

Jadili

1. Kwa maeneo matatu kati ya maeneo ya msingi manne, taja angalau kipimo 1 kilichothibitishwa kimaandishi kuwa na vigezo muhimu vya kuwa kipimo. Kazi hii inatuhitaji tutambue na kufafanua vigezo vya vipimo muhimu, na kuandika ni kwa kiwango gani vipimo vyetu vya msingi vinakidhi vigezo. Kwa kufanya kazi hii, tutatambua mapungufu na fursa za kuendelea kuboresha vipimo vyetu muhimu.

Wazo letu la kuanzia ni kwamba mahitaji ya vipimo muhimu ni pamoja na kwamba vipimo vinatumika kisayansi au kwa uthabiti na vina ufafanuzi wazi, hesabu, asili ya data, matoleo na msimamizi wa data. Tunapoanza kutekeleza vipimo hivi, tunaweza kutambua seti iliyorekebishwa ya vigezo ambavyo vitasaidia zaidi katika kuongoza uteuzi na ufafanuzi wa vipimo.

4. Juhudi mbalimbali za Mipango mitano ya kila mwaka ya hujihusisha na kipimo cha msingi kama hatua ya uchunguzi, kupima na kuwasilisha maendeleo, au kutoa taswira ya mwelekeo wa rasilimali. Tunaweza kutambua kwamba viongozi na wafanyakazi wanaelewa jinsi vipimo vyetu vya msingi vya mpango wa kila mwaka vinavyounganishwa na kazi zao kwa kuzingatia kuwa vipimo hivi vinaathiri mipango ya kila mwaka ya Shirika. Ushawishi unaweza kutofautiana kutoka timu moja hadi timu nyingine na mpango hadi hatua, kwa hivyo tunatafuta viashirio vinavyojumuisha viwango vitatu vya kujihusisha na vipimo hivi. Baadhi ya viongozi wanaweza kujihusisha na vipimo kama zana ya uchunguzi na kufungua uchunguzi ili kuelewa uhusiano wa mitindo na mipango yao ya kila mwaka. Wengine wanaweza kutumia vipimo hivi kama zana ya kuwasiliana kwa upana maendeleo au misingi inayozunguka kazi yao, kama vile kujumuisha vipimo katika ukaguzi wa kila robo mwaka au katika shughuli za mpango wa kila mwaka na harakati. Katika hali nzuri zaidi, viongozi wa mipango ya kila mwaka hutumia moja kwa moja vipimo hivi ili kuongoza na kutathmini maamuzi ya rasilimali, kama inavyoonyeshwa katika mawasiliano ya ndani au nje kuhusu maamuzi haya. Kwa kuhimiza utumiaji huu wa viwango mbalimbali wa vipimo vya msingi vya mpango wetu wa kila mwaka katika mipango mbalimbali ya kila mwaka, tunasogeza shirika zima karibu na ubora wa kutumia seti iliyoshirikishwa ya vipimo ili kuongoza kazi iliyoratibiwa kote kwenye Shirika.

SDS2: Kufanya maamuzi ya kitaalamu

Wafanyakazi wa Wikimedia na uongozi hufanya maamuzi yanayotokana na data kwa kutumia vipimo muhimu ili kutathmini maendeleo ya programu na kutathmini athari.

Muktadha: Kwa kutumia vipimo muhimu kutathmini maendeleo ya programu na kutathmini athari, tunaweza kuhakikisha kuwa tunafanya maamuzi sahihi ambayo yanaungwa mkono na ushahidi. Hii huturuhusu kusalia kulenga malengo yetu muhimu zaidi, kufanya marekebisho inavyohitajika, na kufuatilia maendeleo yetu baada ya muda. Ili kufikia utamaduni huu unaoendeshwa na data, lazima tuanze kwa kuratibu vipimo muhimu na michakato inayohusiana katika zana na matokeo ambayo huwezesha hadhira kuu kuelewa, kutathmini na kuchunguza data ambazo ni za ubora wa hali ya juu. Hii itamaanisha sio tu kuwekeza katika uundaji wa zana za kukagua vipimo, lakini pia kuwekeza katika miundomsingi ya data na masuluhisho ya ubora yatakayotuwezesha kuboresha usahihi, matumizi na kwa muda mwafaka wa bidhaa zetu za data. Tutajikita katika maeneo mawili muhimu:

  • Kuwezesha uongozi mkuu kufanya maamuzi yanayotokana na data kwa kutoa zana na data za pamoja ili kufahamisha mtazamo wao. Kazi hii itajumuisha kufanya vipimo 3 vya msingi vipatikane kama bidhaa za data, kutoa zana zinazoruhusu hadhira husika kuchanganua na kutathmini vipimo hivi, na uwekezaji unaohitajika katika miundombinu ya data na bidhaa zilizopo za data.
  • Kuboresha uzalishaji wa data zinazohusiana na bidhaa na vipengele vyetu vinavyotuwezesha kulinganisha na kuendesha majaribio na bidhaa. Majaribio yanatusaidia kujifunza kwa haraka na hutusaidia kukuza aina zinazofaa za matumizi na jumuiya. Kadiri bidhaa zetu zinavyokua, tunahitaji kubuni mkakati wa kuthibitisha kwa utaratibu na kwa uwazi kwamba maamuzi na uwekezaji wetu unatupeleka katika mwelekeo sahihi wa kushughulikia malengo ya harakati.

Jadili

5. Timu nne za vipengele hutumia zana zilizoshirikishwa kutathmini na kuboresha matumizi ya mtumiaji kulingana na data ya majaribio kutoka kwa mwingiliano wa watumiaji. Kuunda zana zinazoshirikishwa ambazo timu zinazoshughulikia vipengele zinaweza kutumia kupima athari za mabadiliko ya vipengele kutaboresha ufanisi wetu kwa kupunguza juhudi zinazohitajika ili kuunda na kunasa vipimo na kurahisisha kupangilia vipimo hivyo kwenye vipimo vyetu vya msingi.
6. Uongozi mkuu unaweza mara kwa mara kutumia zana iliyoshirikishwa kutathmini maendeleo ya Shirika dhidi ya vipimo vya msingi. Tunapopanga viongozi wakuu kuhusu vipimo vya msingi kama sehemu ya Lengo la 1, tunahitaji kutoa zana zilizo rahisi kutumia zinazowawezesha kutathmini na kupima maendeleo ya Shirika dhidi ya vipimo vya msingi. Kazi hii inachunguza jinsi tunavyoweza kufanikisha hili kupitia ripoti tuli, zana za kuona data, n.k., pamoja na uwekezaji katika miundombinu na ubora wa data. Kwa mwaka huu, lengo letu litakuwa katika kutoa vipimo vya msingi.

SDS3: Kutumia na kusambaza data

Watumiaji wanaweza kufikia kwa uaminifu na kuuliza maudhui ya Wikimedia kwa kiwango kikubwa

Muktadha: Njia zinazowasilisha data kutoka kwenye miradi yetu ni muhimu kwa maendeleo yenye mafanikio ya uzoefu wa kwenye tovuti za Wiki na vile vile kwa zana za maendeleo, uchambuzi wa miradi yetu na shughuli zingine za harakati. Ni lazima tuweze kutoa data kupitia bidhaa za data ambazo ni za kutegemewa, endelevu, na zinazoweza kupanuka ili kukidhi mahitaji ya usambazaji wa maarifa bila malipo, ugunduzi, uhifadhi na uundaji. Eneo muhimu la kuzingatiwa kwa Shirika mwaka huu litakuwa ni kuchunguza jinsi tunavyoweza kutoa suluhisho endelevu zaidi la grafu ya maarifa ambayo inaendelea kusaidia upatikanaji na ukuaji wa maudhui ya maarifa kwa njia ambayo ni endelevu na tendaji, huku tukibakiza ufikiaji wa maudhui yaliyopo. Kwa mwaka huu tujikita zaidi kwenye:.

  • Kuchunguza mbinu za kuboresha utendajikazi wa WDQS na uimara wake
  • Kushughulikia hatari zinazoweza kujitokeza papo kwa papo za kushindwa kufanya kazi zinazohusiana na WDQS
  • Kuweka msingi wa suluhu za muda mrefu za kuongeza grafu ya maarifa inayokua kwa kasi

Jadili

1. Grafu ya maarifa ya Wikidata inaweza kupakiwa upya ndani ya siku 10 kwa grafu ya hadi data bilioni 20 za upili. Suala la msingi ambalo tunajaribu kushughulikia ni uimara wa muda wa kati na uthabiti wa Huduma ya Maulizo ya Wikidata, ambao unaweza kuzuia uwezo wa kuuliza Wikidata. Huduma ya Maulizo ya Wikidata inaendesha juu ya Blazegraph, na inajumuisha data bilioni 15 za utatu. Kwa sasa Grafu inakua kwa kasi data za utatu bilioni 1 kwa mwaka. Kwa ukubwa wa sasa na ukuaji wa grafu, tunakumbana na masuala kadhaa ya upanuzi:
  • Kupakia upya (ujenzi mpya) wa grafu kutoka kwenye madampo ya Wikidata huchukua zaidi ya miezi 2. Kwa sehemu hii ni kwa sababu operesheni ni ndefu, hata hivyo muda umeongezwa kwa sababu upakiaji upya huacha kufanya kazi bila kutabirika pindi tu grafu inapofikia ukubwa fulani, na hivyo kuhitaji mchakato kuwashwa upya.
  • Masuala ya uthabiti ya mara kwa mara na WDQS
  • Maulizo yanachukua muda mrefu zaidi kufanyiwa kazi, na mara nyingine kunashindwa kufanya kazi

Uwezo wa kupakia upya grafu ni kazi muhimu ili kuhakikisha uwiano wa data na kuweza kurejesha matatizo yanayoweza kutokea ya data muhimu. Ni dalili ya uthabiti na uimara wa mfumo. Zaidi ya hayo, ukosefu wa uthabiti wa mchakato wa kupakia upya data unahusishwa moja kwa moja na ukubwa wa grafu, kwa njia sawa na kwamba uthabiti wa wakati wa utekelezaji wa WDQS unaunganishwa na ukubwa wa grafu.

Malengo v2 (v1) Matokeo Muhimu Maelezo Utafiti

FA1: Elezea mikakati mbalimbali inayoweza kutokea

Ambayo kwayo Wikimedia inaweza kukidhi lengo letu la kuwa muundombinu muhimu wa mfumo ikolojia wa maarifa bila malipo

Jadili

1. Washiriki katika kazi ya Hadhira ya baadaye wametayarishwa na angalau mikakati mitatu ya watahiniwa wa jinsi miradi ya Wikimedia (hasa Wikipedia na Wikimedia Commons) itakavyobaki kuwa "miundombinu muhimu ya maarifa bila malipo" katika siku zijazo, ikijumuisha hadhira ambayo ingewafikia, dhana wanazozijaribu, na mbinu za kuzijaribu. Kabla ya Hadhira ya hapo baadae kuchunguza kazi inayoweza kufanywa siku za usoni, tunataka kuweka mikakati mbalimbali ambayo tutakuwa tukiichunguza, na kutafakari maswali ambayo yanahitaji kujibiwa ili kutambua uwezekano wake.

Wanajamii wa Commons wametuuliza kwa uwazi kuhusu mkakati wa siku zijazo wa mradi wa Commons -- KR hii inahakikisha kwamba tunafanya hivyo, lakini pia inalingana na mkakati mkubwa wa bidhaa unaofikiriwa kwenye ndoo.

Muhtasari wa Mitindo ya Nje ya Wikimedia kwa mwaka 2023 uliangazia idadi ya mabadiliko kwenye teknolojia na tabia ya watumiaji katika utafutaji na uundaji wa maudhui ambayo yanahatarisha uendelevu wa harakati zetu. Ufuatiliaji huu wa kazi utalenga kuzama zaidi katika jinsi miradi na jumuiya zetu zinavyoweza kuendelea kustawi katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kutokea siku zijazo.

Mawasiliano: User:MPinchuk (WMF)

FA2: Kujaribu dhana

Kuthibitisha au kubatilisha mikakati inayoweza kutekelezwa kwa siku zijazo, kwa kuanzia na kulenga mifumo ya maudhui ya watu wa upande wa tatu

Jadili

1. Kujaribu dhana inayolenga kufikia hadhira ya vijana duniani ambako wako kwenye majukwaa yanayoongoza ya maudhui ya wahusika wa upande wa tatu, ili kuzalisha mawazo ya bidhaa tunazoweza kutengeneza kwenye au nje ya tovuti zetu, ambayo yanaweza kusaidia kuongeza ushiriki wao kwenye maudhui ya Wikimedia kama watumiaji na wachangiaji. Mojawapo ya maelekezo ya kimkakati ambayo tuna uhakika tunataka kuchunguza ni kuhusu uenezaji wa maarifa bila malipo kwenye mifumo mingine, kama vile YouTube, Instagram, n.k. Kiasi kikubwa cha maarifa kinatumika katika maeneo hayo bila malipo, na bado hatujafanya jambo lolote kuwezesha hilo, wala bado hatuna nadharia za jinsi ya kupata washiriki na mapato kutoka sehemu hizo.

Lugha ya KR hii ilisasishwa mnamo Oktoba 11, 2023 ili kuweka wazi kwamba madhumuni ya KR hii ni kueneza maudhui ya Wikimedia kupitia majukwaa ya watu wengine, kinyume na chapa ya Wikimedia, na kuweka wazi kuwa hii ni katika huduma ya kukuza mawazo ya bidhaa. Maudhui yanapoenea, bado ni muhimu kwamba sifa na chapa kuenea nayo, ili Wikimedia iweze kudumishwa na wahariri na wafadhili -- lakini huo sio msingi wa mwelekeo wa kazi hii.

  • Utafiti wa uhai wa chapa wa mwaka 2022 uliangalia jinsi Wikipedia inavyoonekana na vikundi vya umri tofauti tofauti. Ilibainisha alama za chini hasa kati ya vijana wa miaka 18-24 katika baadhi ya masoko (Marekani, Ujerumani, Afrika Kusini), ambao waliipa Wikipedia Alama hasi ya utumiaji. Kulingana na utafiti huu: "Hii inaleta hatari kubwa kwa mustakabali wa mradi na harakati kwa ujumla."
  • The New York Times liliripoti juu ya ushahidi kwamba vijana duniani wanazidi kutumia muda kwenye programu za kijamii na muda mchache kutumia injini za utafutaji za kitamaduni (ambazo kwa kawaida huleta idadi kubwa ya watazamaji wapya kwenye miradi yetu).

Mawasiliano: User:MPinchuk (WMF)

2. Pima nadharia kuhusu mazungumzo ya kutafuta maarifa kwa njia ya Akili bandia (AI), kuchunguza jinsi watu wanavyoweza kugundua na kujihusisha na maudhui kutoka kwenye miradi ya Wikimedia. Mwelekeo mwingine wa kimkakati ambao tuna uhakika tunataka kuuchunguza ni kuhusu akili bandia ya kimazungumzo, teknolojia ambayo inaonekana kama italeta mageuzi katika mfumo ikolojia wa maarifa bila malipo. Sio zote zinazofanya kazi kwa kutumia miundo mikubwa ya lugha na roboti za kuchati zinaweza kuingia katika matokeo haya muhimu; badala yake ni kazi hiyo tu inayochunguza akili bandia ya mazungumzo kama njia ya kuleta maarifa ya bure kwa hadhira ambayo vinginevyo isingepitia maudhui ya Wikimedia.
  • Reuters liliripoti kuwa kufikia Februari 2023, miezi 2 baada ya kuzinduliwa, ChatGPT ilikuwa na watumiaji hai milioni 100, ikionyesha mvuto wake mkubwa na ukuaji wa haraka.
  • GPT-4 na LLM zingine sasa zinatumika kuwasha zana nyingi mpya ikiwa ni pamoja na za utafutaji na kuunda maudhui mtandaoni. Wengi katika harakati zetu wanavutiwa na wanajali kuhusu jinsi kazi na miradi yetu inavyoweza kuendelea kustawi katika ulimwengu wa zana za kisasa za akili bandia (AI).

Mawasiliano: User:MPinchuk (WMF)