Kanuni Majumui za Maadili/Miongozo ya utekelezaji iliyorekebishwa/Tangazo/Upigaji Kura 1
Kura ijayo juu ya Miongozo ya Utekelezaji iliyorekebishwa ya Kanuni Majumui za Maadili
Habarini nyote,
Katikati ya Januari 2023, Miongozo ya Utekelezaji ya Kanuni Majumui za Maadili itapigiwa kura ya pili ya uidhinishaji katika jamii nzima. Hii inafuatia kura ya Machi 2022, ambayo ilisababisha wapigakura wengi kuunga mkono Miongozo ya Utekelezaji. Wakati wa kupiga kura, washiriki walisaidia kuangazia maswala muhimu ya jamii.Kamati ya Masuala ya Jamii ya Bodi iliomba kwamba maeneo haya husika yakaguliwe.
Kamati ya Marekebisho yakujitolea ilifanya kazi kwa bidii kukagua maoni ya jamii na kufanya mabadiliko. Walisasisha maeneo husika, kama vile mahitaji ya mafunzo na uthibitisho, faragha na uwazi katika mchakato, na usomaji na tafsiri ya hati yenyewe.
Miongozo ya Utekelezaji iliyorekebishwa inaweza kutazamwa hapa, na ulinganisho wa mabadiliko unaweza kupatikana hapa.
Jinsi ya kupiga kura?
Kuanzia Januari 17, 2023, upigaji kura utakuwa wazi. Ukurasa huu kwenye Meta-wiki unaonyesha maelezo kuhusu jinsi ya kupiga kura kwa kutumia SecurePoll.
Nani anaweza kupiga kura?
Masharti ya kustahiki kwa kura hii ni sawa na uchaguzi wa Bodi ya Wadhamini ya Wikimedia. Tazama ukurasa wa maelezo ya mpigakura kwa maelezo zaidi kuhusu ustahiki wa mpiga kura. Ikiwa wewe ni mpiga kura anayestahiki, unaweza kutumia akaunti yako ya Wikimedia kufikia seva ya kupiga kura.
Ni nini kitatokea baada ya kupiga kura
Kura zitachunguzwa na kundi huru la watu wa kujitolea, na matokeo yatachapishwa kwenye Wikimedia-l, Jukwaa la Mkakati wa Harakati, Diff na kwenye Meta-wiki. Wapiga kura wataweza tena kupiga kura na kushiriki mambo walio nao kuhusu miongozo. Bodi ya Wadhamini itaangalia viwango vya usaidizi na hoja zinazotolewa wanapoangalia jinsi Miongozo ya Utekelezaji inapaswa kupitishwa au kuendelezwa zaidi.
Kwa niaba ya Timu ya Mradi wa UCoC,