Mpango wa Mwaka wa Wikimedia Foundation/2025-2026/Malengo na Matokeo Muhimu ya Bidhaa na Teknolojia
This content is currently in development as part of the 2025–2026 Annual Plan drafting process. We are seeking input on questions that will shape the Wikimedia Foundation's priorities for the next fiscal year. |

Mpango wa Mwaka ni maelezo ya Wikimedia Foundation ya kile tunachotarajia kufikia katika mwaka ujao.Tunafanya kazi kwa bidii ili kufanya mpango kuwa shirikishi, wenye matamanio na kufanikishwa. Kila mwaka, tunawaomba wachangiaji kutoa mitazamo yao, matumaini na maombi mahususi tunapounda mpango. Baadhi ya njia tunazotafuta maoni ni kupitia mazungumzo ya timu ya bidhaa na jumuiya, Orodha ya Matamanio ya Jumuiya, mazungumzo ya jumuiya kama vile mfululizo wa mazungumzo ya Commons, kwenye mikutano, na kupitia kurasa za wiki kama huu.
Kwa mpango wetu ujao wa mwaka, kuanzia Julai 2025 hadi Juni 2026, tunafikiria jinsi tunavyoweza kutumikia vyema maono ya vizazi vingi, ukizingatia mabadiliko ya haraka katika dunia na mtandao na jinsi hiyo inavyoathiri dhamira yetu ya maarifa huria.
Kama nilivyosema mwaka jana, tunahitaji kuangazia kile kinachotutofautisha: uwezo wetu wa kutoa maudhui ya kuaminika hata kama taarifa potofu na mbaya zinapoenea kwenye mtandao na kwenye majukwaa yanayoshindania umakini wa vizazi vipya. Hii ni pamoja na kuhakikisha tunafanikisha dhamira ya kukusanya na kutoa jumla ya maarifa yote ya binadamu kwa ulimwengu kwa kupanua wigo wetu wa taarifa zinazokosekana, ambazo zinaweza kusababishwa na ukosefu wa usawa, ubaguzi na upendeleo. Maudhui yetu yanahitaji pia kutumika na kubaki kuwa muhimu katika mabadiliko ya intaneti yanayoendeshwa na akili mnemba na uzoefu tele. Na hatimaye, tunahitaji kutafuta njia za kufadhili harakati zetu kwa uendelevu kwa kujenga mkakati wa pamoja wa bidhaa zetu na kukusanya pesa ili tuweze kusaidia kazi hii kwa muda mrefu.
Ili kufanya chaguo na maelewano kuhusu mahali pa kuelekeza juhudi zetu katika mwaka ujao, tulikusanya maswali pamoja na kufikiria jinsi ya kutenga rasilimali zetu zenye kikomo ili kupata matokeo makubwa zaidi.
Ikiwa una nia mahususi katika sifa au huduma ambazo idara ya Bidhaa na Teknolojia itaunda kulingana na vipaumbele vilivyowekwa hapa, kutakuwa na wakati Machi wa kutoa maoni kuhusu malengo mahususi na matokeo muhimu. (Haya hapa ni malengo na matokeo muhimu ya mpango wa sasa wa mwaka, kwa marejeo.)
Iwapo ungependa kufikiria kuhusu changamoto na fursa katika mazingira yetu ya kiufundi na mwelekeo tunaopaswa kuweka katika mpango ujao wa mwaka, tafadhali zingatia maswali yaliyo hapa chini pamoja nasi.
Tunaendelea kupokea taarifa kuhusu maswali haya kwa njia nyingi -- kutoka mazungumzo ya jumuiya, data tunazokusanya, mahojiano ya utafiti tunayofanya, na zaidi. Hii si mara ya kwanza tunauliza na kujifunza kuhusu mengi ya mambo haya–na tayari tumekuwa tukifanya kazi karibu na wengi wao! Tunataka kuwauliza tena sasa na kuendelea kujifunza, kwasababu ni wa umuhimu kwetu katika hatua hii ya upangaji wetu.
Maswali:
- Vipimo na data
- Ni njia zipi ambazo data na vipimo vinaweza kusaidia vyema kazi yenu kama wahariri? Unaweza kufikiria data kuhusu kuhariri, kusoma, au kupanga ambazo zingeweza kukusaidia kuchagua jinsi ya kutumia wakati wako, au wakati jambo fulani linahitaji kushughulikiwa? Hii inaweza kuwa data kuhusu shughuli yako mwenyewe au shughuli za wengine.
- Uhariri
- Ni wakati gani ambapo kuhariri kunakufaa zaidi na kukufurahisha? Ni wakati gani inakatisha tamaa na ngumu zaidi?
- Tunataka wachangiaji wapokee maoni zaidi na kutambuliwa kwa kazi zao, ili isionekane kama hakuna mtu anayetambua juhudi wanazotumia kwenye wiki. Ni aina gani ya maoni na utambuzi yanayokupa hamasa? Ni nini kinachokugusa uendelee kuhariri?
- Kwa sababu wiki ni kubwa sana, inaweza kuwa vigumu kwa wahariri kuamua ni kazi gani ya wiki ni muhimu zaidi kwao kutumia muda wao kila siku. Ni habari au zana gani zinaweza kukusaidia kuchagua jinsi ya kutumia wakati wako? Je, ingeweza saidia kuwa na sehemu kuu, ya binafsi ambayo inakuruhusu kupata fursa mpya, kudhibiti kazi zako na kuelewa matokeo yako?
- Tunataka kuboresha uzoefu wa ushirikiano kwenye wiki, ili iwe rahisi kwa wachangiaji kutafutana na kufanya miradi pamoja, iwe ni kupitia hifadhi rudufu, warsha za hariri, Miradi ya Wiki, au hata wahariri wawili wanaofanya kazi pamoja. Unafikiri tunaweza kuwasaidia vipi wachangiaji zaidi kutafutana, kuunganika na kufanya kazi pamoja?
- Kusoma/Kujifunza
- Wiki hupakia haraka au polepole kulingana na mahali ambapo watu wanaishi ulimwenguni. Je, kuna sehemu yoyote duniani ambapo unafikiri kwamba utendakazi ulioboreshwa unahitajika zaidi?
- Tunawezaje kusaidia vizazi vipya vya wasomaji kupata maudhui ya Wikipedia ya kuvutia na shirikishi? Tumejadili mawazo kuhusu maudhui na video zenye mwingiliano hapo awali, na katika mwaka huu tumeangazia kwenye chati na kwenye kujaribu njia mpya za kuibua yaliyomo kwenye Wikipedia. Je, tunawezaje kuendelea na mwendo huu ili kutumia maudhui yetu yaliyopo kwa njia mpya ambazo ni za kipekee kwa Wikimedia?
- Wasimamizi
- Ni nini kinachoweza kuhitaji kubadilishwa kuhusu Wikipedia ili watu wengi zaidi watake kujihusisha katika majukumu ya juu ya kujitolea, kama vile wafanya doria au wakabidhi?
- Ni taarifa au muktadha gani kuhusu hariri au watumiaji unaweza kukusaidia kufanya doria au maamuzi ya mkabidhi kwa haraka au kwa urahisi zaidi?
- Mitindo ya Nje
- Ni mabadiliko gani muhimu zaidi unayoona duniani nje ya Wikimedia? Hizi zinaweza kuwa mitindo ya teknolojia, elimu, au jinsi watu wanavyojifunza.
- Nje ya harakati za Wikimedia, ni jumuiya gani nyingine za mtandaoni unazoshiriki? Tunaweza kujifunza nini kutoka kwenye zana na michakato kwenye majukwaa mengine ya jumuiya?
- Unatumia vipi zana za AI ndani na nje ya kazi yako ya Wikimedia? Je, unaona AI inakufaa kwa nini?
- Commons
- Ni maamuzi gani tunaweza kufanya na jumuiya ya Commons ili kuunda mradi endelevu unaosaidia kuunda maarifa ya ensaiklopidia?
- Wikidata
- Ungependa kuona Wikidata inakua vipi katika siku zijazo? Je, inawezaje kuwa muhimu zaidi kwa ajili ya kujenga maudhui ya ensaiklopidia ya kuaminika?